Wananchi
wa kijiji cha Katulukila kata ya mkula wilaya ya Kilombero mkoani
Morogoro wameiomba serikali kuingilia kati mgogoro uliopo baina yao na
mwekezaji aliyevamia hekari zaidi ya 500 za msitu wa hifadhi ya
Magombera unaomilikiwa na kjiji hicho chini ya mamlaka ya uhifadhi
wanyamapori ya Selou.
ITV imefika katika kijiji cha katulukila na kushuhudia uharibifu
uliofanywa na mwekezaji huyo ambaye amekuwa akifanya shughuli za kilimo
cha mpunga,upasuaji wa mbao pamoja na uchomaji wa mkaa ambapo wananchi
wamelalamikia serikali kushindwa kuonesha jitihada za kunusuru hifadhi
hiyo.
Naye mhifadhi mkuu wa kanda ya Msolwa Agustino Ngamilanga amesema
mamlaka haitavumilia kuendelea kufanyika uharibifu wa hifadhi hiyo kwani
inahifadhi viumbe adimu ambavyo havipatikani mahali pengine duniani.
Akijibu malalamiko ya wananchi hao mwekezaji wa shamba hilo amesema
anamiliki kihalali shamba hilo na kwamba wakati anaendelea na
uzalishaji katika eneo hilo kesi ya msingi inayohusu mgogoro wa shamba
hilo inaendelea katika baraza la ardhi la wilaya ya Kilombero.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini