WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali haijaridhia viwango vipya vya nauli ya mabasi yaendayo kasi vilivyopendekezwa na waendeshaji wa huduma ya mabasi yaendayo kasi Dar es salaam (UDART).
Akizungumza
leo na waandishi wa habari, mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam
akitokea mkoani Ruvuma kwa ziara ya siku 3, Waziri Mkuu amesema Serikali
haijaridhia viwango vipya vya nauli ya mabasi yaendayo kasi. Ambapo
nauli ya kutoka Mbezi hadi Kimara shilingi 700, Mbezi hadi Kariakoo
shilingi 1200, na nauli ya kutoka Mbezi hadi Mwenge shilingi 1400 na
wanafunzi watatozwa nusu ya viwango hivyo vya nauli.
Waziri
Mkuu amesema gharama hizi ni kubwa mno kwa wananchi na watumishi, mradi
ulilenga kumrahisishia mtumishi wa Serikali anayeishi nje ya jiji, “Serikali iliwekeza katika mradi huu ili kusaidia watumishi na wananchi ambao hawana vipato vikubwa” alisema Waziri Mkuu.
Aidha,
ameagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa George Simbachawene na Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi,
na Mawasiliano pamoja na wadau wakutane kupanga upya viwango hivyo na kama watashindwa basi Serikali itaendesha mradi huo.
Tarehe
25, Novemba 2015, Waziri Mkuu alimuagiza aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara
ya TAMISEMI na waendeshaji wa mradi wa mabasi yaendayo kasi Dar es
salaam (UDART) kupitia misuada yote na kurekebisha miundombinu ili mradi
huo wa mabasi uanze kufanya kazi ifikapo tarehe 10, Januari 2016,
imebainika kwamba UDART hawakuandaa mpango wa biashara wala kuanisha
gharama za uendeshaji.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini