Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimsalimia Josephine John ambaye amelazwa
katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma kwa matibabu. Alikuwa katika ziara ya
mkoa huo Januari5, 2016.
********
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amewaonya Madaktari vinara wa Hospitali ya Rufaa
ya Songea ambao wanasifika kwa kufanya biashara ya kutoa mimba wanawake
na wanafunzi kuacha tabia mara moja,lasivyo atawafukuza kazi na kuwafunga jela.
Waziri
Mkuu alitoa onyo hilo jana wakati alipotembelea Hospitali hiyo na
kuzungumza na watumishi kwa lengo la kuwasisitiza kutoa huduma bora kwa
wagonjwa,ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 3 mkoani Ruvuma.
Alisema Hospitali ya mkoa huo inasifika kwa kutoa mimba wanawake na kuwalaza wagonjwa wao wodi namba 5, kitendo ambacho serikali haikuruhusu wala haikubaliani nacho.
"Naomba
mkuu wa mkoa fanya ziara ya kushtukiza katika wodi namba 5 utakuta
wanawake wametolewa mimba, wakiwemo wanafunzi na kisha madaktati hao
wanatumia wodi zetu kuwalaza wagonjwa wao waliowatoa mimba.Ni marufuku
na nitawachukulia hatua kwani majina ya madaktari hao ninayo," alisisitiza majaliwa.
Waziri
Mkuu Majaliwa alimuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa huo,Dr. Daniel Malekela na
Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dr. Phils Nyimbi kuwafuatilia
madaktari wanaojihusisha na vitendo hivyo na kutoa taarifa ili
wachukuliwe hatua kali.
Pia,
alimuagiza mganga mkuu Dkt Daniel Malekela kuondoa duka lake lililo
jirani na hospitali hiyo ili kuondo hisia kwamba dawa zinaibiwa na
kupelekwa kwenye maduka ya watumishi.
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na Madaktari na Wauguzi wa Hospitali
ya Mkoa wa Ruvuma baada ya kuitembelea akiwa katika ziara ya mkoa huo
Januari 5, 2016.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo, Thabiti Mwabungu na kulia
ni Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na bibi Antonia Moyo ambaye alikuwa
akipata matibabu katika chumba maalum cha waze katika hospitali ya mkoa
wa Ruvuma wakati alipoitembelea hositali hiyo akiwa katika ziara ya mkoa
huo Januari 5, 2016. Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo Thabiti Mwabungu.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa,akimsalimia mtoto Flora Mapunda (1) ambaye
amelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma ambayo Waziri Mkuu
aliitembelea na kuzungumza na watumishi akiwa ktika ziara ya mkoa huo
Januari 5, 2016 Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini