Makamu
wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan
amewaonya baadhi ya watumishi wa sekta ya afya nchini kujiepusha na
tabia ya kuuza dawa zinazopelekwa na serikali kwenye zahanati, vituo vya
afya na hospitali kwani hali hiyo inaweza kusababisha manung’uniko kwa
wagonjwa na wananchi kuichukia serikali yao.
Alitoa
onyo hilo jana alipotembelea na kuzindua majengo ya hospitali teule ya
Rufaa ya mkoa wa Geita, yaliyokarabatiwa kwa ushirikiano kati ya
serikali ya Tanzania na mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) kwa gharama ya
jumla ya shilingi milioni 271, ambapo mgodi wa GGM umechangia shilingi
milioni 212 na serikali imetoa shilingi milioni 59.
Kwa
upande wake waziri wa afya, maendeeleo ya jamii, jinsia, wazee na
watoto Mh. Ummy Mwalimu alikiri kuwepo kwa wizi pamoja na upotevu wa
dawa za serikali kutokana na kukosekana kwa uwajibikaji na uadilifu
miongoni mwa watumishi wa sekta ya afya.
Hospitali
hiyo teule ya Rufaa ya mkoa wa Geita inatarajiwa kuhudumia zaidi ya
watu 1,700,000 wanaoishi katika mkoa huo kwa mujibu wa sensa ya mwaka
2012, kabla ya kuwa hospitali ya rufaa ilikuwa ikihudumia zaidi ya watu
laki nane wa halmashauri ya Geita.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini