Mfanyakazi wa ndani anadaiwa kujiua kwa kujinyonga kwa kutumia mtandio kwenye nyumba ya mwajri wake iliyopo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Ofisa
Mtendaji wa Kata ya Iringo, Asia Temu alisema mfanyakazi huyo alijiua
hivi karibuni bila ya kuacha ujumbe wowote kuhusiana na sababu za
kuchukua uamuzi huo.
Temu
alisema tukio hilo liligundulika baada ya mtoto mdogo wa mfanyakazi
huyo aliyemtaja kwa jina la Zatila Said kuhitaji huduma kutoka kwa mama
yake na kuanza kulia kwa kutomuona.
Alisema
kutokana na hali hiyo, mtoto wa mwenye nyumba, Wendelini Dominick (8)
alichukua jukumu la kumtafuta mfanyakazi huyo ndani ya nyumba yao na
kumkuta amekufa kwa kujinyonga.
Mwajiri wa mfanyakazi huyo, Dominick Papaa alisema alijinyonga wakati akiwa kazini na mkewe.
Kamanda
wa Polisi mkoani Mara, Phillip Kalangi alisema hakuna mtu
anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo na kusisitiza wanafanya uchunguzi
kubaini chanzo chake.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini