
Watu
29 wamelazwa katika hospitali ya Mrara ya halmashauri ya mji wa Babati
mkoani Manyara baada ya kugundulika kuugua ugonjwa wa kipindupindu, huku
wataalam wa afya wakidai kupatwa na hofu ya huenda idadi kubwa ya
wagonjwa ikaendelea kuongezeka kutokana baada ya kupokea wagonjwa 18
siku tatu zilizopita na hadi kufikia saa sita mchana ya leo (alhamisi)
idadi hiyo imeongezeka toka wagonjwa 28 hadi kufikia 29.
Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Bw Gabriel Sonno Amekiri kupokea
idadi hiyo ya wagonjwa na kuthibitisha ukweli kwamba wanasumbuliwa na
ugonjwa wa kipindupindu baada ya kufanyika kwa uchunguzi wa kitaalam
uliotokana na kupokea wagonjwa wanaohara mfululizo na kutapika, idadi ya
wagonjwa 26 wakiwa wanaume na wanawake watatu, huku akisisitiza kwamba
hakuna mtu aliyepoteza maisha tangu walipoanza kupokea wagonjwa tangu
siku ya jumatatu.
ITV imetembelea ndani ya wadi hiyo na kushughudia idadi kubwa ya
wagonjwa wengine wakiwa wamelazwa chini na wengine kwenye ukumbi wa
ushauri wa akinamama wajawazito na upimaji wa watoto (MCH), huku
wagonjwa hao wakieleza chanzo cha ugonjwa wa kipindupindu ni kula kwa
mama lishe mmoja kwenye kituo cha mabasi ambaye mpaka sasa wafanyakazi
wake watatu wamelazwa huku yeye akisalimika.
Nae Bw Faustine Masunga, mkuu wa usafi na mazingira katika
halmashauri ya mji wa Babati, amesema licha ya kufunga vibanda vya
biashara za vyakula kwa siku 14 na sasa fursa pekee iliyopo ni kusimamia
usafi wa mazingira na kusimamia kikamilifu sheria zilizopo ili
kudhibiti mlipuko huo ambao haujawahikutokea na kulazwa idadi kubwa ya
wagonjwa kama hiyo tangu kuanzishwa kwa mkoa wa Manyara, Julai mosi,
2002.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini