
Katika kikao kilicho wakutanisha kamati ya ulinzi na usalama wilaya
ya Babati wawakilishi wa wakulima wafugaji na wajumbe wa serikali ya
kijiji mkuu wa wilaya ya Babati Crispin Meela amesema baada ya
kutafakari kwa muda mrefu athari wanazo zipata wananchi hasa wafugaji
serikali imeamua kuwapatia eneo ilo wafugaji ili kumaliza mgogoro uliyo
ghalimu muda uhai na uchumi wa binadamu bila sababu ya msingi.
Awali kabla ya kauli ya mkuu wa wilaya Mpama ardhi wa wilaya ya
Babati Bryceson Shesha alitoa matokea ya kamati iliyoundwa kutazama
enelo walilo pewa wafugaji ambalo awali walilikataa kuwa halifai kwa
makazi na mifugo na kwamba watalam wamelipitia na kuona kuwa linafaa
japo kuna changamoto ndogondogo na wawalishi wa wafugaji nao wakieleza
kuridhishwa na hatua hiyo na kutakiwa kupeleka tamko ilo kwa wafugaji
waliyo wengi ili nao watambue kinacho endelea.
Baada ya makubaliano hayo diwani wa kata ya Nkaiti kutoka Chadema
Michael Melau akaitaka serikali kutimiza ahadi hiyo haraka kwani watu wa
jamii ya kifugaji katika eneo ilo wameteseka kwa muda mrefu hivyo
watendaji wasije wakabadili mpango huo kwa manufaa binafsi.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini