Viongozi
wa Kitongoji cha Kasalazi, kilichoko katika Kijiji cha Kanyara, Kata ya
Bulyaheke, wilayani Sengerema, Mkoa wa Mwanza, wanadaiwa kuwachapa
fimbo hadharani wanawake wanaovaa nguo fupi zinazoonyesha baadhi ya
sehemu zao za siri.
Pia,
viongozi hao wanadaiwa kuwatoza faini ya Sh 20, 000 wanawake wanaokutwa
na nguo hizo kama njia ya kuwafanya wasiendelee kuvaa nguo hizo.
Mmoja
wa wasichana waliowahi kuchapwa na viongozi hao aliyejitambulisha kwa
jina la Juliana Mafuru, alichapwa fimbo baada ya kufika kijijini hapo
kwa lengo la kununua dagaa.
“Cha
kushangaza ni kwamba, baada ya kufika katika kitongoji hicho, mgambo
walinikamata na kunichalaza bakora mbele za watu nje ya boti niliyokuwa
nimepanda.
“Pia waliamuru nivue suruali niliyokuwa nimeivaa na kuanza kuichana chana nyembe.
“Wakati
wananifanyia hivyo, walitokea wasamalia wema ambao walinipatia shuka la
kimasai ili niweze kujisitili, yaani waliniabisha kweli.
“Baadaye, walinipeleka kwenye ofisi ya kitongiji hicho na walinitoza faini ya shilingi 20,000, kisha wakaniachia,” alisema Juliana.
Nao
wakazi wa kijiji hicho, Lafael Bitulo na Mariamu Chacha, walisema
mwenyekiti wa kitongiji hicho na katibu wake, ndiyo vinara wa tabia hiyo
kwa kuwa wamekuwa wakinufaika nayo.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Kitongoji hicho, Andrea Mkama, alikiri
kuwachapa fimbo wanawake wanaovaa nguo fupi na zinazobana kwa mavazi
wanayovaa ni ya udharirishaji.
Naye
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kanyara, Lazoro Mgonzo,
alithibitisha wanawake kuchapwa fimbo ingawa alisema ni kitendo cha
udharirishaji.
Mkuu wa Wilaya Sengerema, Zainabu Terack alipoulizwa juu ya tukio hilo, alisema hana taarifa ingawa aliahidi kulifuatilia
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini