Jeshi la Polisi Idara ya Uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam linawashikilia watu 39 katika oparesheni ya kuwakamata wahamiaji haramu wanaofanya kazi na biashara zinazoweza kufanywa na watanzania kwenye eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Wakati huohuo linawashikilia watanzania wawili waliobainika kufanya biashara ya usafirishaji haramu wa watanzania nje ya nchi.
Oparesheni hiyo imefuatia siku chache baada ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Yussuf Masauni kubainisha kuwa inalenga kuwakamata na kuwafikisha mahakamani, kisha kuwarejesha katika nchi zao, wageni hao wanaoishi huku wakifanyakazi na biashara kinyume cha sheria au kufanya shughuli zinazoweza kufanywa na watanzania.
Miongoni mwa waliokamatwa katika oparesheni hiyo ni Raia wa China 25, Waghana 3, Wakongo 3, Wanigeria 3, Wasomali 3, Ivory Cost 1, Mzimbambwe mmoja na watanzania wawili.
Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar Es Salaam Masumule anasema Oparesheni hiyo ni endelevu na jeshi hilo limejipanga kikamilifu kuitekeleza.
Miongoni mwa waliokamatwa wamebainika kuishi nchini bila hati za kusafilia , huku wengine wakiishi bila vibali, licha vibali vyao kuisha muda na kufanya shughuli zinazoweza kufanywa na wazawa .
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini