Mfumuko Wa Bei 2015 Tathmini yaonesha kupungua kwa asilimia 5.6. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Saturday, January 9, 2016

Mfumuko Wa Bei 2015 Tathmini yaonesha kupungua kwa asilimia 5.6.



Ofisi ya Taifa ya Takwimu imetoa tathmini ya mfumuko wa bei kwa mwaka uliopita wa 2015 ambao umepungua kwa asilimia 5.6 kutoka asilimia 6.1 kama ilivyokuwa mwaka 2014.
Mkurugenzi wa Sensa ya watu na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo amesema kupungua kwa mfumuko wa bei katika kipindi cha mwaka jana kulichangiwa na kushuka kwa kasi ya kupanda kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo amesema mfumuko wa bei zisizo za vyakula ulipungua mpaka asilimia1.8 kwa mwaka 2015 kutoka asilimia 4.9 ya mwaka 2014
Ndipo akafafanua mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwezi ambao umeongezeka kwa asilimia 0.5 ukilinganisha na ongezeko la asilimia 0.8 mwezi November 2015
Amesema mfumuko wa bei nchini una mwelekeo unaofanana na baadhi ya nchi nyingine za Afrika Mashiriki, ambapo kwa Kenya umeongezeka kwa asilimia 8.01 kutoka asilimia 7.32 kwa mwaka 2015 na Uganda umeongezeka hadi asilimia 9.30 kutoka asilimia 9.18.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin