ITV imeshuhudia wagonjwa hao wakiwa wamelala wawili hadi watatu
huku baadhi yao wakiwa sakafuni baada ya kukosa viatanda vya kuwalaza
hatua ambayo mkuu wa kituo hicho Sister Matilda Shirima amesema hatua
hiyo inatokana na ongezeko la wagonjwa ambapo wanaofika kuripoti kwa
siku wanafikia 5000 hadi 6000 na wale wanaolazwa ni zaidi ya 45 hadi 60
kwa siku.
Baadhi ya wagonjwa waliokutwa katika kituo hicho wameziomba taasisi
zilizo na zisizo za kiserikali kusaidia changamoto wanazokabiliana nazo
wagonjwa hasa akina mama na watoto kwa sababu wengi wao wanatembea
umbali mrefu kufuata huduma katika kituo hicho lakini wanalazimika
kulala sakafuni huku wengine wakilala wawili hadi watatu kufuatia
vitanda kujaa wagonjwa.
Kufuatia hatua hiyo mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) tawi la
Korogwe umesaidia kupunguza sehemu ya changamoto hizo ikiwemo mashuka
kufuatia baadhi ya wagonjwa wanaolala sakafuni kukosa hata nguo za
kujifunika hatua ambayo imekuwa ikiathiri afya zao.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini