
Mvutano huo ulianza mapema asubuhi baada ya waziri mwenye dhamana
husika kuwasilisha kauli yake bungeni kuhusu matangazo hayo hatua ambyo
iliharibu hali ya hewa na kusababisha kikao kuahirishwa ili kutoa mwanya
wa kamati ya uongozi kuka na kufanya maamuzi.
Hata hivyo bunge hilo lilirudi kwenye kikao chake cha jioni ambapo
hali ilizidi kuwa mbaya baada ya mwenyekiti Chenge kutangaza kuwa kamati
ya uongozi ya bunge imesema ratiba ya kikao cha bunge iendele kama
kawaida na ndipo hali ikanza hivi.
Tafurani hiyo ikadumu kwa muda mrefu na ndipo polisi wakaingia ndani kwa lengo la kuwatoa nje wabunge.
Kama vile haitoshi hata waandishi wa habari nao walitolewa nje na
mkuu wa kitengo cha habari elimu na mawasiliano kwa umma Bw Owen
Mwandumbya hatu ambayo ili walazimu wanahabari kushindwa kutekeleza
majukumu yao.
Awali kabla ya vurugu hizo baadhi ya wabunge wamepokea kwa mitizamo tofauti kauli ya serikali.
Badhi ya wabunge ambao ni wanataaluma ya habari wamesemakitendo cha
kuzuia kutangaza bunge ni hatua ya mwanzo ya kuuwa uhuru wa habari
nchini na hivyo serikali inabidi kujitazama upya.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini