
Licha
ya kuhusishwa na uchafu, na mazingira duni, kunguni ameibuka kuwa mdudu
mwenye uwezo mkubwa wa kustahimili hatari dhidi ya maisha yake.
Utafiti
mpya umebaini kuwa wadudu hao wanaweza kustahimili sio tu tanuri ya moto
na baridi kali bali pia madawa ya kisasa ya kuua wadudu wanaotambaa.
Kunguni
wamegundulika kuwa wanaweza kustahimili kupuliziwa dawa nyingi ya sumu
kwa kuimarisha uwezo wake wa kujikinga dhidi ya sumu moja baada ya
nyengine.
Wadudu
hao ambao huishi kwa kufyonza damu ya wenyeji wake wakiwa usingizini
wanauwezo mkubwa wa kibayolojia ya kujikinga dhidi ya sumu kali.
Hii ni
kusema kuwa kadri vizazi vya kunguni vinavyopuliziwa madawa yenye sumu
ndivyo wadudu hao wanavyoimarisha uwezo wake wakuzuia maafa miongoni mwa
watoto wao.
Aidha,
watafiti wanaema kuwa vipimo 1000 vya sumu kali aina ya (neo-nicotinoid)
vinahitajika kuua kunguni mmoja huko Marekani katika majimbo ya
Cincinnati na Michigan ikilinganishwa na maeneo mengine duniani.(VICTOR)

Watafiti
wanasema vipimo 1000 vya sumu kali vinahitajika kuua kunguni mmoja
katika majimbo ya Cincinnati na Michigan ikilinganishwa na maeneo
mengine duniani Watafiti hao sasa wanasema kuwa kuna hatari kubwa ya
mdudu huyo kuenea kote duniani kutokana na utandawazi na soko huria
ambao umefanya ulimwengu kuwa kitongoji kikubwa tu.
Aidha
wanasayansi hao wanashauri kutafutwa mbinu tofauti na mpya ya
kukabiliana na kunguni pasi na kutumia sumu, kama vile kutafuta wadudu
wengine wanaoweza kuwala ilikuzuia wadudu hao kuenea kote duniani.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini