Takwimu:Nchi za Africa zawa vinara kwa ufisadi Duniani. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Thursday, January 28, 2016

Takwimu:Nchi za Africa zawa vinara kwa ufisadi Duniani.




Tanzania yashika nafasi ya 117 kwa ufisadi Duniani.
Tanzania yashika nafasi ya 117 kwa ufisadi Duniani.
Takwimu za hivi punde zinaonesha taswira mbaya kuhusiana na kuzorota kwa maadili na uadilifu miongoni mwa viongozi wengi wa Afrika na haswa kusini mwa jangwa la Sahara.
Takwimu hizo zaidi zinaonesha kuwa ufisadi umesakama uchumi wa mataifa 40 kati ya 46 Kusini mwa jangwa la Sahara, katika kanda ya Afrika Mashariki, Burundi inaongoza kwa kiwango cha juu zaidi cha Ufisadi ikiorodheshwa katika nafasi ya 150 duniani ikiwa na jumla ya alama 21 pekee.
Uganda na Kenya zimetoshana katika nafasi ya 139 zikiwa na alama 25.
Tanzania ina alama 30 na imeorodheshwa katika nafasi ya 117 duniani.
Rwanda ndio taifa lililoongoza katika kanda hii ya Afrika kwa kupigana na ufisadi, inaalama 54 na imeorodheshwa katika nafasi ya 44 duniani.
Botswana ndio inayoongoza barani Afrika kwa vita dhidi ya ufisadi, taifa hilo la kusini mwa Afrika lina jumla ya alama 63.
Cape Verde ni ya pili na alama (55), Seychelles ya tatu na alama (55), Rwanda ni ya nne na alama (54), 5;Mauritius (53) nayo Namibia ikiorosheshwa katika nafasi ya 6 na alama (53).
Mkurugenzi wa Transparency International (TI) kanda ya kusini mwa jangwa la Sahara Chantal Uwimana, anasema kuwa kuanzia kwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola hadi kukithiri kwa mashambulizi ya kigaidi bara la Afrika linazidi kujuta kutokana na kukithiri kwa visa vya ufisadi.
haijakuwa mwaka mzuri kwa mataifa ya Afrika na haswa katika mataifa makubwa zaidi kiuchumi barani yaani Afrika Kusini na Nigeria ambapo visa vya ufisadi vimepelekea kuibuka maandamano ya umma na vilevile badiliko la kisiasa kufuatia uchaguzi mkuu nchini Nigeria.
Iwapo Afrika inataka kwa kweli kupigana vita na ubadhirifu wa mali ya umma, na matumizi mabaya ya mamlaka kwa faida ya kibinafsi sharti mataifa ya Afrika yawekeze katika jitihada za kupamabana na ufisadi’, alisema Chantal Uwimana
Somalia ambayo imekuwa bila serikali ya kitaifa tangu mwaka wa 1991 ndio taifa linaloongoza kwa visa vya ufisadi, taifa hilo la upembe wa Afrika linashikilia nafasi hiyo kwa pamoja na taifa la kikomunisti la Korea Kaskazini.
Ripoti hiyo inasema kuwa japo serikali nyingi za Afrika zinajaribu kupunguza vizuizi vya kufanya biashara, wananchi wake hawajabadili mtazamo wao kuhusu maadili.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin