Wakati dunia ikiwa na zaidi ya watu 34 milioni wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU), madaktari nchini Hispania wametangaza kugundua tiba ya ugonjwa huo wanayodai ni uhakika.
Kwa
kutumia damu ya kupandikiza kutoka kwenye kitovu mwana (umbilical cord)
cha mtu ambaye ana vinasaba ambavyo havipokei virusi hivyo vya Ukimwi,
wataalamu hao wa tiba wa Hispania wanaamini kuwa wanaweza kutibu ugonjwa
huo baada ya mafanikio waliyopata kwa mgonjwa mmoja.
Madaktari
hao wa Kitengo cha Taifa cha Upandikizaji (ONT) cha Hispania walichukua
damu ya vitovu mwana vya watu wenye vinasaba ambavyo havipokei VVU na
kuipandikiza kwa mtu anayeishi na virusi hivyo. Baada ya miezi mitatu,
mgonjwa huyo alipimwa na kuonekana hana virusi.
Daktari
wa Programu ya Upandikizaji kutoka Taasisi ya Tiba ya Catalan,
Barcelona, Rafael Duarte alisema mgonjwa aliyetibiwa kwa njia hiyo,
Timothy Brown (37), alikuwa anaishi na VVU tangu mwaka 2009 na madaktari
hao walithibitisha kuwa amepona baada ya kupandikizwa damu hiyo.
Mgonjwa mwingine aliyefanyiwa majaribio ya tiba hiyo alipona VVU, lakini miaka mitatu baadaye alifariki kwa ugonjwa wa saratani.
Timu
ya madaktari wa Hispania ililiambia gazeti la kila siku nchini humo la
El Mundo kuwa wana uhakika kuwa wameleta mapinduzi katika mapambano ya
Ukimwi na magonjwa yanayofanana na hayo.
Dk
Duarte alisema mwaka 2015 umekuwa wa kujivunia ugunduzi huo mkubwa
duniani, ingawa alitahadharisha kuwa tiba kamili haiwezi kupatikana
katika siku za usoni.
Kaimu
mkurugenzi wa mwitikio wa Taifa wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania
(Tacaids), Dk Morris Lekule alisema utafiti kama huo hauna budi kufuata
taratibu zote na kuthibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kabla ya
kutangazwa kuwa ni tiba sahihi.
“Kila
mara taarifa zinakuja zikisema tiba ya Ukimwi imepatikana, lakini tiba
kupata uthibitisho kwamba ni sahihi, ni mchakato mrefu unaotakiwa
kuhakikisha kama kweli dawa hiyo inatibu na ni lazima WHO wathibitishe
hilo,” alisema.
Alisema
ni vizuri kama wataalamu hao wakapata uhakika kutoka WHO badala ya
kuwapa watu matumaini kuwa kuna tiba na baadaye matumaini hayo
yanapotea.
Daktari
wa kitengo kinachoshughulika na masuala ya Ukimwi cha WHO, Richard
Banda alisema hana taarifa za tiba hiyo. Tiba inavyofanya kazi Madaktari
wa ONT walitumia damu ya mtu mwenye vinasaba vya ‘CCR5Delta’ ambavyo
seli zake haziathiriwi na virusi hivyo vya Ukimwi.
Dk
Duarte alisema kwanza huziua seli za damu ya mgonjwa kwa kutumia mionzi
halafu seli mpya (kutoka kwenye damu ya mtu mwenye seli zisizoathiriwa
na VVU hupandikizwa. Damu hiyo ilipandikizwa kwa mgonjwa mwenye virusi
hivyo na saratani ya damu.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini