Waziri
wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mh. Mwigulu Lameck Nchemba, amemfukuza kazi
mkuu wa mnada wa mifugo wa Pugu, na watumishi walioshiriki kuiba ushuru
wa serikali, alipoenda machinjioni hapo kukagua.
Waziri
Nchemba amesema alienda machinjioni hapo kutatua kero zinazowakabili
wananchi na wadau wa machinjio hayo, huku akishirikisha wizara mbili ya
Afya na TAMISEMI.
“Nimerejea
asubuhi ya leo kwenye machinjio ya Vingunguti kwa ajili ya kutatua kero
zinazowakabili watumiaji wa machinjio hayo, kutokana na uwepo wa
ubadhilifu wa kodi ya serikali kwenye mnada wa pugu na malalamiko kadhaa
yanayogusa wananchi wanaotumia machinjio haya, nimeshirikisha wizara
mbili (TAMISEMI na AFYA) kutoa majawabu ya muda mfupi na ya kudumu”, alisema Waziri Nchemba
Baada
ya kufika machinjioni hapo Waziri Mwigulu Nchemba alitoa maagizo kwamba
Mkuu wa mnada wa machinjioni hapo watafute kazi nyingine, na kuwataka
kufika ofisi ya Katibu Mkuu wa wizara.
“Nimeagiza
kuwa Mkuu wa mnada wa Pugu na watumishi waliokuwa zamu tar. 24.12.2015
na tar.01.01.2016, kuanzia sasa watafute kazi nyigine, wakati huohuo
wahakikishe wanafika ofisi ya Katibu mkuu wizarani kwangu mapema
Jumatatu tar.04/01/2016”, alisema Waziri Nchemba.
Pamoja
na hayo Waziri Nchemba amesitisha uchukuaji wa ushuru katika eneo la
mnada wa Pugu, na kutaka makusanyo ya fedha zote yafanyike machinjio ya
Vingunguti kwa kutumia mashine za EFD.
“Kuanzia
sasa nimesitisha uchukuaji wa ushuru eneo la mnada wa Pugu, badala yake
makusanyo yote ya fedha za serikali yatafanyika machinjio ya Vingunguti
kwa kutumia mashine za elektroniki za EFD, kwa maana hiyo mnada wa Pugu
utakuwa unatumika kutoa vibali tu vya mifugo ilikudhibiti ubora wa
mifugo inayopaswa kuchinjw”, alisema Waziri Nchemba.
Pia
waziri Nchemba ametaka eneo la kuhifadhia nyama lililokuwa limejengwa
kwa fedha za wananchi kushirikiana na serikali lifunguliwe kwa ajili ya
wananchi kulitumia kuhifadhia nyama.
Hatua
za kuboresha miundombinu ya machinjio hayo zimeelekezwa kwa Halmashauri
ya Ilala zifanyiwe kazi haraka na kwa ubora, na kutakiwa kurudishwa kwa
umeme uliokuwa umekatwa eneo hilo, kwa ajili ya kuwarahisishia wananchi
shughuli zao.
Mh:Mwigulu
Nchemba akiwa ameambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI
Mh:Simbachawene wakiwasili kwenye eneo la machinjio ya Vingunguti
kwaajili ya kutoa majawabu kutokana na kero mbalimbali zinazowakabili
wadau wa machinjio hayo.Mwigulu
Nchemba akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh:Simbachawene
wakikagua eneo la machinjio ya Vingunguti kabla ya kuzungumza na wadau
wa eneo hilo pamoja na uongozi wake.
Mh:Mwigulu Nchemba akiwa ameongozana na Mh:Simbachawene wakielekea kuzungumza na wananchi wanaotumia Machinjio ya vingunguti.Mawaziri
kutoka kulia ni Naibu waziri wa Afya Mh:Kigwangallah,Wa pili kutoka
kulia ni Mbunge wa Jimbo la Segerea Mh:Bonah,Watatu kutoka kulia ni
Mh:Simbachawene na wa mwisho kushoto ni Mh:Mwigulu Nchemba wakijadiliana
jambo.Mkutano ukiendelea wa kutoa majawabu kuhusu changamoto za Machinjio ya Vingunguti.Mh:Simbachawene
akiwaagiza watumishi wote wa Machinjio ya Vingunguti kuripoti ofisini
kwake Jumanne wakiwa na mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala.Mh:Mwigulu
Nchemba akizungumza na Wananchi(Wadau) wa machinjio ya Vingunguti
kuhusu hatua za kinidhamu alizozichukua kwa Mkuu wa mnada wa pugu
inakotoka mifugo kabla ya kufika Machinjio ya Vingunguti kwa upotevu wa
mamilioni ya shilingi ya kodi za serikali.Mawaziri wakiagana na wananchi mara baada ya mkutano wa kutatua kero zao za Machinjio kumalizika.Furaha
ya Wananchi mara baada ya kutatuliwa kero zao kwa hatua za
awali,wananchi wanasukuma gari la Mh:Mwigulu Nchemba kama ishara ya
kukubali hatua alizochukua.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini