Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameamua kumjibu mgombea urais wa Marekani, Donald Trump ambaye hivi karibuni alidai kuwa akiingia madarakani atahakikisha anawakamata na kuwafunga yeye na rais mwenzake wa Uganda, Yoweri Museveni.
Mugabe
alitumia hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya maendeleo iliyofanyika
jijini Harare juzi (Januari 3) kumjibu Trump. Alisema kuwa Trump ana
damu ya Hitler.
Hivi ndivyo alivyoeleza:
“Hivi
karibuni yule mwendawazimu anayetaka kuwa rais wa Marekani alisema kuwa
atawakamata baadhi ya marais wa Afrika akiwemo kaka yangu Yoweri na
mimi na kutufunga gerezani endapo atakuwa rais.
“Naomba
nimueleze hapa kwamba Trump hataweza kutupeleka popote kwa sababu sisi
waafrika ni imara zaidi duniani na hatuogopi. Ningependa kila mmoja
kufahamu kuwa sina cha kuogopa na nataka niiambie dunia kuwa huyo mzimu
wa Hitler umemchukua na anakaribia kufanya ya hovyo watu wa Marekani
wakimchagua.
“Kama
ambavyo babu yake Hitler alivyosababisha vita ya pili ya dunia, na yeye
anataka kuanzisha vita ya tatu ya dunia ili aache kumbukumbu lakini
dunia haitaruhusu hilo.
“
Hivi inakuaje unaanza hata kufikiria kuwa utamkamata mtu kama mimi? Hivi kichwa cha Trump kiko sawa? Na… hivi kuna madaktari wa kutosha Marekani kumpima ukichaa huyu mtu?
Hivi inakuaje unaanza hata kufikiria kuwa utamkamata mtu kama mimi? Hivi kichwa cha Trump kiko sawa? Na… hivi kuna madaktari wa kutosha Marekani kumpima ukichaa huyu mtu?
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini