Misimu
wa sikuu za Christmas na Mwaka Mpya ilikuwa na neema kwa
wafanyabiashara wengi nchini lakini iliacha vilio vya utapeli kwa baadhi
wa wafanyabiashara hususan maeneo ya pwani waliojikuta wametoa mali
halali na kupewa fedha bandia.
Baadhi
ya wamiliki wa Maduka na watoa huduma za simu pesa wilayani Kibaha
mkoani Pwani wamepata hasara kubwa baada ya kusambaa kwa noti bandia za
shilingi 10,000 katika eneo hilo katika msimu wa sikukuu hizo.
Eneo la Maili Moja na Kibaha ndio maeneo yanayodaiwa kuathirika zaidi na udanganyifu huo wa kutumia noti bandia.
Mmoja
kati ya wafanyabiashara wa Bar, Lubul Lebulu aliwaambia waandishi wa
habari kuwa alibaini kuwa alipoteza shilingi 120,000 wakati akifunga
mahesabu yake ya sikukuu ya Christmas baada ya kubaini kuwa kuna noti
bandia zilizokuwa zimechanganywa na fedha halali.
“Kuna
mzunguko mkubwa wa noti bandia hapa katika eneo letu. Sio mimi pekee,
wafanyabiashara wengi wamepata hasara kama hii. Watu wanapaswa kuwa
makini zaidi kwa sababu suala hilo limeshabainika,” alisema Lubul.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Pwani, Boniveture Munishogi alisema kuwa jeshi hilo
linamshikilia kijana mmoja kuhusiana na tuhuma za kujihusisha na
udanganyifu wa kutumia noti bandia.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini