Shirika hilo linaongeza kuwa uchunguzi wao wa kitaalamu unafanana na ule ambao wameupata kutoka kwa mashahidi kuwa kuna makaburi mengine ya pamoja ya watu waliouwawa siku ya tarehe 11,desemba,siku ambayo ilishuhudia machafuko makubwa mjini Bujumbura.
Ripoti hiyo imekuja siku chache kabla ya mkutano wa viongozi wa umoja wa Afrika kukutana kujadili hatima ya mgogoro wa Burundi huko Ethiopia.
Mgogoro wa Burundi ulianza april mwaka uliopita, wakati ambapo raisNkurusinzinza Pierre alipotangaza kuwania nafasi ya uraisi kwa awamu ya tatu na kuchaguliwa tena kuwa raisi mwezi july mwaka wa jana.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini