Kundi la mawakili,
wanaharakati na wanasayansi nchini Brazil limewasilisha ombi mahakama ya
juu nchini humo likitaka wanawake wenye virusi vya Zika waruhusiwe
kutoa mimba.
Virusi vya Zika vinaaminika kusababisha watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo, na kudumaza ubongo.Utoaji mimba nchini Brazil hauruhusiwi kisheria, ila tu wakati wa dharura ya kiafya au iwapo mimba imetokana na ubakaji hali ambayo kwa Kiingereza inajulikana kama microcephaly.
Hata hivyo mwaka 2012, uliruhusiwa kwa watu walioathiriwa na ugonjwa mwingine wa ubongo kwa jina anencephaly.
Wataalamu wameonya kwamba idadi ya watu walioambukizwa na virusi vya Zika mwaka huu huenda ikafikia kati ya milioni tatu au nne mwaka huu mabara ya Amerika.
Ombi hilo mpya litawasilishwa mahakama ya juu katika kipindi cha miezi miwili.
- “Msishike mimba sasa”, mataifa yashauri wanawake
-
WHO yaeleza wasiwasi kuhusu Zika
- Njia 10 za kujikinga dhidi ya virusi vya Zika
Wanawake wa Brazil “hawafai kuadhibiriwa kutokana na matokeo ya sera dhaifu (za serikali”, kundi hilo linasema.

Hayo yakijiri, Thomas Bach, mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki amesema hatua zinachukuliwa kulinda michezo ya mwaka huu ambayo itaandaliwa mjini Rio de Janeiro.
IOC itatoa mwongozo baadaye Ijumaa kwa wanariadha na wageni ambao wanapanga kushiriki au kuhudhuria michezo hiyo.
Brazil ndilo taifa lililoathirika zaidi na mlipuko wa Zika.
Kuna visa 270 vya watoto kuzaliwa na vichwa vidogo ambavyo vimethibitishwa, kwa mujibu wa wizara ya afya nchini humo.
Kuna visa vingine 3,448 vya microcephaly ambavyo vinachunguzwa.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini