Kwa mara ya kwanza mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amezungumzia suala la mgogoro huo huku akiweka msimao wake kuwa suluhisho lake litafuata katiba na maamuzi ya wananchi. Maalim Seif ametoa tamko hilo hapa Zanzibar wakati akizungumzia katika hafla ya Maulidi ya Mtume Mohamed -SAW-yaliyafanyika katika ukumbi wa Salma na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo rais mstaafu wa Zanzibar wa awamu ya sita Dr Amani Abeid Karume, aliyekuwa mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba na mzee Hasan Nasosr Moyo ambapo amesema suluhisho liko makribu na kuwataka wananchi wasubiri huku akiwahakikishia kuwa suluhisho hilo litakuwa kwa mujibu wa katiba na sheria. Maalim Seif ambaye pia ni makamu wa kwanza wa rais amesisitiza haja ya amani na utulivu na kuwataka wananchi kutulia na kuendeleza amani hiyo huku akiwasihi wanachama wa CUF kuendelea kuwa makini na kutokubali kuchokozwa. Wananachi wa Zanzibar wanaingia katika mwezi wa tatu wakisubiri hatama ya mgogoro huo wa kisiasa huku kila upande ukiwa na misimamo yao kuhusu hatma ya mgogoro wa kisiasa juuya kufutwa kwa uchaguzi mkuu. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Thursday, January 7, 2016

Kwa mara ya kwanza mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amezungumzia suala la mgogoro huo huku akiweka msimao wake kuwa suluhisho lake litafuata katiba na maamuzi ya wananchi. Maalim Seif ametoa tamko hilo hapa Zanzibar wakati akizungumzia katika hafla ya Maulidi ya Mtume Mohamed -SAW-yaliyafanyika katika ukumbi wa Salma na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo rais mstaafu wa Zanzibar wa awamu ya sita Dr Amani Abeid Karume, aliyekuwa mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba na mzee Hasan Nasosr Moyo ambapo amesema suluhisho liko makribu na kuwataka wananchi wasubiri huku akiwahakikishia kuwa suluhisho hilo litakuwa kwa mujibu wa katiba na sheria. Maalim Seif ambaye pia ni makamu wa kwanza wa rais amesisitiza haja ya amani na utulivu na kuwataka wananchi kutulia na kuendeleza amani hiyo huku akiwasihi wanachama wa CUF kuendelea kuwa makini na kutokubali kuchokozwa. Wananachi wa Zanzibar wanaingia katika mwezi wa tatu wakisubiri hatama ya mgogoro huo wa kisiasa huku kila upande ukiwa na misimamo yao kuhusu hatma ya mgogoro wa kisiasa juuya kufutwa kwa uchaguzi mkuu.

    Kwa mara ya kwanza mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amezungumzia suala la mgogoro huo huku akiweka msimao wake kuwa suluhisho lake litafuata katiba na maamuzi ya wananchi.
Maalim Seif ametoa tamko hilo hapa Zanzibar wakati akizungumzia katika hafla ya Maulidi ya Mtume Mohamed -SAW-yaliyafanyika katika ukumbi wa Salma na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo rais mstaafu wa Zanzibar wa awamu ya sita Dr Amani Abeid Karume, aliyekuwa mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba na mzee Hasan Nasosr Moyo ambapo amesema suluhisho liko makribu na kuwataka wananchi wasubiri huku akiwahakikishia kuwa suluhisho hilo litakuwa kwa mujibu wa katiba na sheria.
 
   Maalim Seif ambaye pia ni makamu wa kwanza wa rais amesisitiza haja ya amani na utulivu na kuwataka wananchi kutulia na kuendeleza amani hiyo huku akiwasihi wanachama wa CUF kuendelea kuwa makini na kutokubali kuchokozwa.
 
  Wananachi wa Zanzibar wanaingia katika mwezi wa tatu wakisubiri hatama ya mgogoro huo wa kisiasa huku kila upande ukiwa na misimamo yao kuhusu hatma ya mgogoro huo ambapo umetokana na kufutwa kwa uchaguzi mkuu na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jecha Salum Jecha.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin