Wakati operesheni ya kuweka alama ya X kwenye nyumba zilizojengwa mabondeni, maeneo ya wazi na kinyume na taratibu ikiendelea, Hoteli za Double Tree na Slip Way nazo zimekumbwa na pigo hilo.
Hoteli
hizo pamoja na nyumba ya Maheshbhai Patel na baadhi ya wamiliki wengine
wa nyumba ambao kuta zake zimejengwa karibu na barabara ya Slip Way
eneo la Msasani Peninsula, wamepewa siku saba kuzibomoa.
Jana,
uongozi wa Manispaa ya Kinondoni uliweka alama za X na kuwaonya
wamiliki hao kwamba, wasipobomoa manispaa itazibomoa na kudai gharama za
ubomoaji.
Akizungumza
kwa simu jana, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William
Lukuvi alisema Serikali haitaurudi nyuma katika kutekeleza sheria hata
kama kuna watu wana jeuri ya pesa.
Alisema
Manispaa ya Kinondoni iliwapatia vibali vya kupendezesha maeneo ya
pembezoni mwa barabara ikiwamo kupanda maua, lakini wao badala ya
kutimiza masharti ya vibali walizungushia kuta jambo ambalo
hawatalivumilia.
“Wangependezesha
na kufunga minyonyoro kuzuia kuharibiwa mazingira yao kama walihisi
wananchi wangeharibu, lakini siyo kujenga kuta.
“Nimewaagiza Kinondoni wawapatie notisi ya siku saba kubomoa kwa hiari. Wasisubiri Serikali ivunje.
"Tutabomoa hadi lile jengo lililopo karibu na Hospitali ya Ami lililovunja sheria, yule hawezi kuonyesha jeuri ya fedha,” alisema Lukuvi.
Alisema
Serikali ina mpango maalumu wa kubomoa majengo yote yaliyojengwa
kinyume na sheria Masaki na Oysterbay na wameanza na Barabara ya Slip
Way.
Katika
hatua nyingine, sakata la bomoabomoa pia limewakumba waliojenga katika
hifadhi za mikoko baada ya watumishi wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira
(NEMC) na maofisa misitu wa Manispaa ya Kinondoni kuweka alama ‘X’
katika nyumba zaidi ya 30 ikiwamo ya kiongozi wa Kanisa la Mikocheni B
Assemblies of God, Dk Getrude Rwakatare.
Kazi
hiyo ilianza jana mchana katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam
ikiwamo, katika Mtaa wa Ally Sykes, Kawe na Jangwani Beach eneo la Mbezi
Beach. Ofisa Misitu Msaidizi wa Manispaa ya Kinondoni, Issa Juma
aliwaambia wanahabari kuwa kazi hiyo ni endelevu.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini