Bajeti ijayo kuongeza kivuko kimoja Kigamboni. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Wednesday, January 13, 2016

Bajeti ijayo kuongeza kivuko kimoja Kigamboni.


Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Pro. Makame Mbarawa amesema ili kukabiliana na uvujaji wa mapato katika vivuko vya Kigamboni serikali itaanzisha mfumo mpya ya uvushaji wa magari pamoja na ulipaji tiketi.
Mhandisi Karim Mattaka (katikati) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (kushoto)
Prof Mbarawa amesema hayo jana wakati alipofanya ziara katika kivuko cha Kigamboni/Magogoni jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa mfumo huo utawezesha abiria waweze kulipia huduma hiyo kwa mwaka kwa wale wenye uwezo huo.
Aidha Pro. Makame amekiri kuwepo kwa mapungufu katika vivuko hivyo ikiwemo eneo dogo la kusubiria abiria pamoja na miundo mbinu ya walemavu hivyo kuwataka TEMESA kuboresha hali hiyo.
Aidha Waziri Mbarawa ameongeza kuwa katika kuendelea uboreshaji wa vivuko hivyo Serikali imepanga katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha kununua kivuko kingine na kufanya vivuko kuwa vitatu ili kukidhi mahitaji ya wananchi wanaotumia usafiri huo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin