Serikali kuwatoza Kodi wamiliki Nyumba za Kupangisha | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Wednesday, January 13, 2016

Serikali kuwatoza Kodi wamiliki Nyumba za Kupangisha


 Image result for mbeya jiji
SERIKALI imesema inaandaa utaratibu utakaowabana wamiliki wa nyumba binafsi za kupangisha kulipa Kodi ya Mapato kama wafanyabiashara wengine kwa sababu wanaingiza kipato kisicholipiwa kodi.
Utaratibu huo unaandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakianza kwa kuwatambua Wamiliki wa nyumba zote zinazoendesha biashara hiyo kote nchini.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dokta Ashatu Kijaji, amebainisha mpango huo wa Serikali wakati akizungumza na Waandishi wa habari jijini Mbeya na kusema Serikali imedhamiria kukusanya kodi kutoka kwa wamiliki wa nyumba hizo.
Kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakijiuliza kwa nini Serikali haikusanyi kodi kutoka kwa Wamiliki wa nyumba za makazi wanaozipangisha kwa watu wengine, mapato ambayo yanayonekana kupotea bure bila ya kukusanywa na mamlaka husika, swali ambalo huenda sasa likapatiwa majibu na Serikali ya awamu ya Tano.
 Mmoja kati ya wakazi wa jiji la Mbeya amesema fedha hizo ni mapato ya nchi yanayopaswa kukusanywa ipasavyo.
Suala la wamiliki wa nyumba za kupanga kulipa kodi ni mjadala wa muda mrefu kutokana na wamiliki hao kupata mapato kupitia tozo la pango la kila mwezi kutoka kwa wapangaji wao mapato ambayo yanapaswa kulipiwa Kodi kama inavyoeleza Sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 2004.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin