Watu 2 wamekufa na wengine 12 wamelazwa baada ya kuugua ugonjwa wa kipindupindu Kigoma. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Wednesday, December 16, 2015

Watu 2 wamekufa na wengine 12 wamelazwa baada ya kuugua ugonjwa wa kipindupindu Kigoma.


Watu wawili wamekufa na wengine 12 wamelazwa katika zahanati ya kijiji cha Kagunga katika halmashauri ya wilaya ya Kigoma baada ya kuugua ugonjwa wa kipindupindu huku ikielezwa kuwa asilimia 25 ya kaya katika halmashauri za mkoa wa Kigoma hazina vyoo.
Akitoa tathmini ya shughuli za usafi katika mkoa wa Kigoma, mganga mkuu wa mkoa wa Kigoma Dk Lenard Subi amesema kutokana na kushamiri kwa kipindupindu mkoani Kigoma kwa miaka mingi, mkoa umeweka mikakati kadhaa ya kukabiliana na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa kila kaya inakuwa na choo na kukitumia baada ya kubainika kaya nyingi hasa za mwambao wa ziwa Tanganyika hazina vyoo na badala yake watu wanajisaidia katika ziwa Tanganyika na kwamba kila alhamisi imepangwa kuwa siku ya usafi katika mkoa wa Kigoma. 
 
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wameshauri halmashauri kutunga sheria ndogo ili kuweka mkazo wa usafi katika kila halmashri na kwamba jukumu la kupambana na kipindupindu ambacho kimedumu kwa muda mrefu mkoani Kigoma linapaswa kuishirikisha jamii ili itimize masharti ya afya.
 
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin