Na Jacquiline Mrisho-Maelezo
SERIKALI
kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi
imewaasa vijana waliomaliza shule kuacha kujibetweka bali watumie elimu
waliyoipata kujitafutia ajira ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu
wa ajira nchini.
Kauli
hiyo imetolewa jana Jijini Dar es Salaam na Kaimu Kamishna wa Elimu
kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi,
Nicholaus Bureta wakati wa ufunguzi wa mkutano wa vijana wa Afrika
unaojadili changamoto zinazowakabili vijana katika nyanja mbalimbali za
maendeleo.
Bureta
alisema kuwa Serikali inatoa elimu bora ili kuhakikisha vijana
wanapata uwezo na maarifa yatakayowasaidia kujiajiri hata wasipopata
nafasi za kuajiriwa katika taasisi na ofisi za umma pamoja na kuitumia
elimu hiyo katika kupambana na vitendo vya rushwa.
“Sera
ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 inatutaka tuwe na watanzania
walioelimika na wenye mtazamo chanya ambao utahakikisha jamii yetu
inabadilika kufikia uchumi wa kati hivyo vijana msikae kusubiri ajira
bali mjifunze jinsi ya kujiajiri kutokana na elimu mliyoipata
mashuleni”, alisema Bureta.
Kwa
upande wake Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa (UN), Stellah Vuzo
aliwapongeza vijana hao kuamua kukusanyika kuchangia mawazo yao juu ya
matatizo yanayowakabili kwani vijana wana nafasi kubwa ya kuhakikisha
malengo mbalimbali yanatekelezeka.
Aidha,
aliongeza kuwa Umoja wa Mataifa umemteua balozi kijana ambaye
anashughulikia ajira za vijana hivyo aliwaomba vijana walioshiriki
katika mkutano huo kuyafikisha mawazo hayo kwa balozi huyo ili yaweze
kupatiwa ufumbuzi.
Naye
Mkuu wa Utafiti kutoka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (PCCB),
Daniel Pundu alisema kuwa tatizo la rushwa haliwezi kuisha endapo vijana
hawatashirikishwa hivyo amewasisitiza vijana kushirikiana na Serikali
kuchukua hatua za kupambana na rushwa ili kuhakikisha rushwa inaondoka.
“Tunajua
kuwa vijana ndio nguvu kazi ya Taifa na ndio sababu tunawasisitiza
kupambana na rushwa, kwa kulitambua hilo Serikali imeanzisha vilabu vya
wapinga rushwa katika shule za sekondari na vyuo vikuu vikiwa na lengo
la kuhakikisha vijana wanahusika kwenye mapambano hayo”, alisema Pundu.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini