Kukosekana
kwa fedha ya kukamilisha mchakato wa sheria ya Parole kwa wafungwa
mbalimbali nchini waliomaliza nusu ya kifungo chao gerezani ni miongoni
mwa sababu yakuwepo mrundakano wa wafungwa katika magereza Tanzania.
Akiongea na waandishi wa habari hii jana
jijini Dar es salaam wakati akimpongeza na kisha kumteua Mchungaji Dkt.
Getrude Lwakatare kuwa mratibu wa harambee ya kuchangisha fedha
kwaajili ya kuwalipia wafungwa wanaotakiwa kutoka gerezani chini ya
sheria ya Parole, Mwenyekiti wa bodi ya Parole Taifa Augustino Lyatonga
Mrema alisema ili mfungwa atolewe gerezani ni lazima maofisa wa parole wafuatilie nakala ya hukumu.
“Ni
lazima maofisa wa parole wafuatilie nakala ya hukumu kwenye mahakama
iliyomukuhumu na waende kuonana na uongozi wa kijiji au mtaa ambapo
mfungwa atenda kuishi anapotoka gerezani ikiwa ni pamoja na kuonana na
familia yake na pia kuonana na watu waliowakosea ili jamii ya eneo hilo
itambue kuwa ataachiwa huru” alisema
Aidha, Mrema aliwataka
maofisa wa parole kote nchini kuwatembelea wafungwa waliopata Parole
ili wafungwa wengi wenye sifa za kutolewa kwa sheria ya Parole
wasiendelee kuteseka magerezani bali waende kuungana na familia zao
sambamba na kuongeza nguvu kazi.
Kutokana
na kutotengwa fedha kwaajili ya kushugulikia suala hilo, Mwenyekiti
huyo wa Parole Taifa, amemteua Mama Getrude Lwakatare kuwa mratibu wa
kuchangisha fedha kwa kushirikisha viongozi wote wa dini nchini
kushiriki harambee kwaajili ya kuchangisha fedha za kuwatoa wafungwa
magerezani na kupunguza msongamano katika magereza nchini.
“Napendekeza
kufanyike harambee kwenye makanisa yote nchini, siku ya Jumapili moja
ili sadaka zote zikatumike kuwalipia faini wafungwa waliopo magerezani” alisema
Mrema alisisitiza kuwa wanaolengwa na Parole siyo wanye makosa ya ubakaji, mauaji, wizi kwa kutumia silaha na makosa mengine.
Naye Mchungaji Dkt. Getrude Lwakatare aliwataka
watanzania kuangalia taifa kwanza kwani kina baba wengi wenye nguvu
watarudi katika jamii na kusaidia katika uzalishaji mali sambamba na
kutatua matatizo ya kiuchumi na kimaendeleo katika familia zao.
“Tutaunganisha
familia zilizo sambaratika na kutaabika baada ya mzazi mmoja kufungwa
miaka 6 pengine kwa kukosa faini ya milioni moja tuu, tutaondoa
msongamano wa wafungwa na kulinda afya zao kutokana na magonjwa
wanayopata wakiwa gerezani” alisema
Mchungaji Gutrude Lwakatare alisema
anaunga mkono jitihada za bodi ya Parole Taifa na siyo kuwalinda
waalifu kama ambavyo wengine watatafsiri kwani kurejesha familia ni
miongoni mwa kustawisha jamii huku akinukuu maneno ya kidini yanayolenga
kuwakomboa walioko kwenye vifungo na taabu mbalimbali ndani ya jamii.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini