Aliyekuwa
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa jimbo la Misungwi,
Charles Kitwanga (CCM) amezungumzia jinsi alivyopokea kutumbuliwa kwake
na Rais John Magufuli ambaye anaamika kuwa rafiki yake akisema hawezi
kuhoji uamuzi huo.
Kitwanga
aliwaaambia waandishi wa habari nyumbani kwake Misungwi kuwa ingawa
hawezi kuhoji uamuzi huo, kuna kundi kubwa la wauza madawa ya kulevya
ndio waliolikuza tukio hilo kwa lengo la kumchongea hadi kuondolewa
kwenye nafasi hiyo.
“Anayofanya
Dk. Magufuli nampongeza sana kwani ni mtu ambaye namfahamu. Ni
mwadilifu, msikivu, namshukuru kwa kuniamini kufanya kazi naye katika
Serikali yake hivyo siwezi kuhoji alichoamua kwa sababau aliyetoa ndiye
aliyeondoa,” alisema Kitwanga.
Katika
hatua nyingine, Mbunge huyo wa Misungwi alikana kuhusika kwa namna
yoyote katika sakata la kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd iliyopewa
zabuni ya kufunga mashine za kutambua alama za vidole kwenye vituo vya
polisi nchini, na kudaiwa kulipwa kiasi kikubwa cha fedha wakati kazi
haikufanyika kama ilivyotarajiwa. Sakata hilo bado lipo katika uchunguzi
japo dalili za kujadiliwa bungeni zinaonekana kufifia.
“Rais
wa Kwanza wa Tanzania hayati Mwalimu Julius Nyerere, kuna wakati
alituhumiwa akidaiwa kuwa na mpango wa kumpindua Rais wa Kenya baada ya
kuzuru nchini humo. Alipoulizwa na waandishi wa habari alijibu, ‘hivi
mtu akikwambia mimi ni mume wa mama yako utakubali?’, sasa hilo ndilo
jibu langu kwa Watanzania ili wasiniulize tena,” alisema Kitwanga.
Akizugumzia
umiliki wa kampuni ya Infosys, alisema kuwa yeye ni mwanzilishi tu wa
kampuni hiyo na hivi sasa inamilikiwa na mwanae baada ya kumuuzia
asilimia 33 ya hisa zake na kwamba taarifa ya mauzo hayo ziko wazi.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini