BENKI
ya NMB kwa mwaka jana imepata faida ya Sh. Bil. 150.2 kiwango ambacho
ni kikubwa kuliko benki yoyote hapa nchini, faida hiyo ni zaidi ya
asilimia 33 ya faida yam waka 2015 kwa benki zote.
Hayo yameelewa na Mkurugenzi wa NMB – Ineke Bussemaker katika Mkutano Mkuu wa 16 wa wanahisa wa benki hiyo uliofanyika jumamosi jijini Dar es Salaam, huku benki hiyo ikiainisha mafanikio makubwa kwa mwaka 2015 na maono ya mafanikio zaidi kwa mwaka 2016 matumaini ambayo wanahisa waliyapokea kwa mikono miwili.
Katika
mkutano huo, wanahisa walipitisha gawio la shilingi Bilioni 52 ambapo
kila hisa itapata gawio la shilingi 104. Kwa maana hiyo, serikali
itapata gawio la shilingi Bilioni 16.5 kama gawio la hisa zake 31.8
wanazomiliki kwenye benki ya NMB.
Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas alisema "Tuna
furaha kwamba benki imeendelea kuimarika kifedha katika kasi ile ile
iliyopita, na nguvu ya ukuaji imezidi kuwa juu na kuongezeka kwa
asilimia 18, hivyo kutanua thamani ya jumla ya taasisi hii, ikiwa ni
pamoja na tahamni ya hisa zenu,"
Alifafanua
ya kwamba, NMB imeendelea pia kutanua soko na pato katika mikopo na
amana, na kwamba pato litokanalo na riba lilikua kwa asilimia 5 kutoka
Sh. Bil. 417 mwaka 2014, hadi kufikia Sh. Bil. 438 kwa mwaka uliopita wa
2015.
"Licha
ya faida ya jumla kuu kushuka kulinganisha na mwaka jana, lakini gawio
la Wanahisa litabaki kama lilivyokuwa, ambako kila hisa moja itakuwa na
thamani ya shilingi 104, uamuzi ambao ulifurahiwa na kupongezwa na
wanahisa walioshiriki mkutano huo," alisema.
Alivitaja
baadhi ya vikwazo vya maendeleo ya benki hiyo mwaka jana kuwa ni pamoja
na mzunguko finyu wa pesa kutokana na harakati za Uchaguzi Mkuu,
kushuka mara kwa mara kwa thamani ya shilingi katika soko la
kubadilishia fedha.
Barnabas
aliongeza kuwa, moja ya masuala muhimu ambayo NMB ilijikita kuyafanyia
kazi mwaka jana ni pamoja na kumalizia uboreshaji matawi 98 waliyoachiwa
na NBC ambayo yalikuwa katika hali mbaya na kuhamisha Makao Makuu ya
Benki hiyo.
Aliongeza
kuwa, katika kipindi cha miaka 10 sasa, NMB imejipambanua kama kinara
miongoni mwa taasisi za kifedha, na kwamba moja ya ubinafsishaji ulioipa
Serikali faida ni pamoja na wa benki hiyo.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa NMB, Ineke Bussemaker akizungumza na Msajili wa
Hazina, Lawrence Mafuru kabla ya kuanza kwa Mkutano Mkuu wa 16 wa mwaka
wa benki hiyo uliofanyika, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika
mkutano huo, wanahisa walibariki gawio la shilingi bilioni 52
lililotokana na faida ya shilingi Bilioni 150.2 ya faida baada ya kodi
iliyoipata benki ya NMB ambapo Kila hisa itapata gawio la shilingi 104
kiwango ambacho ni cha juu kuliko benki yoyote nchini.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa NMB Ineke Bussemaker,azkingumza na Mwenyekiti wa Bodi,
Profesa Joseph Semboja wakati wa Mkutano wa 16 wa benki hiyo
uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni kwa wiki.Katika mkutano huo,
wanahisa walipitisha gawio la shilingi Bilioni 52 baada ya kupata faida
baada ya kodi ya shilingi Bilioni 150.2 kwa mwaka 2015. Kwa gawio Hilo,
Kila hisa itapata gawio la shilingi 104 kiwango ambacho ni cha huu
kuliko benki yoyote nchini
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa NMB, Ineke Bussemarker kwenye mkutano na waandishi wa
habari baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa 16 wa benki hiyo. kushoto
ni Ofisa Mkuu wa Fedha wa NMB(chief finance officer), Waziri Barnabas.
Mkurugenzi wa NMB alikuwa akitangaza maazimio ya wanahisa ambao
walipitisha gawio la jumla la shilingi Bilioni 52 lililotokana na faida
ya shilingi Bilioni 150.2 na hivyo Kila hisa ikipata gawio la shilingi
104 kiwango ambacho ni cha juu kabisa kuliko benki nyingine yoyote.
Mwisho
Leo ndio siku ya mwisho ya kununua Hati Fungani ya NMB. Tembelea tawi lolote la NMB au piga simu 0800 11 22 33
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini