Wanachama wakubwa 17 wa CHADEMA mkoani Kagera wahamia CCM. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Wednesday, June 15, 2016

Wanachama wakubwa 17 wa CHADEMA mkoani Kagera wahamia CCM.



Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)katika wilaya ya Karagwe iliyoko mkoani Kagera kimepata pigo kwa kuondokewa na wanachama 17 waliokuwa wapiga debe maarufu wa chama hicho wilayani humo waliotangaza kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM).
 Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kukabidhi kadi za uanachama wa CHADEMA kwa Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Kagera,Bi.Costancia Buhiye wamesema wameamua kuihama CHADEMA na kujiunga na CCM baada ya kuridhishwa na utendaji wa kazi wa Rais wa awamu ya tano Dkt.John Pombe Magufuli kwa kuwa mambo waliyokuwa wakiyataka ndio yanafanywa na Rais huyo.
 
Naye,Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Kagerabi.Costancia Buhiye  akizungumza baada ya kuwapokea wanachama hao waliojiunga na chama amesema CCM kitaendelea kuwapokea wote waliokuwa wamepotea hasa waliokuwa wamejiunga kwenye chama icho kwa ushabiki.
 
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin