Waziri wa fedha
nchini Uganda Matia Kasaija amesema kuwa maafisa huenda wakafutwa kazi
iwapo watapatikana wamefanya safari zisizo na maana kwa kutumia fedha za
serikali.
Tangazo hilo ni miongoni mwa hatua za kubana matumizi ya fedha za serikali ili kusaidia kufadhili miradi mingineBungeni,Bw Kasaija aliangazia kuhusu bajeti kubwa ya serikali inayogharimu dola bilioni 8 katika kipindi cha fedha cha mwaka ujao.
Anataka kuimarisha matumizi kuhusu ujenzi wa miundombinu na kuwekeza katika kilimo,utalii,biashara na teknolojia.
Lakini amesema kwamba hakutakuwa na kodi mpya na hivyobasi kuibua maswali vipi taifa hilo litaweza kujimudu.
Njia mojawapo ni serikali kuongeza kukopa.Bajeti hiyo inakasoro ya takriban dola bilioni 4.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini