Rais
mstaafu Benjamini Mkapa ametetea uamuzi wake wa kuruhusu ubinafsishwaji
wa baadhi ya taasisi za umma, huku pia akikiri baadhi ya kasoro
zilizojitokeza wakati wa zoezi hilo ambapo pia ametumia fursa hiyo
kuwataka wasomi kuacha kulalamika na badala yake kutumia muda mwingi
kufanya tafiti zenye manufaa mapana kwa taifa.
Licha ya kuwataka wasomi kuacha kulalamika, rais mstaafu Benjamini
Mkapa pia amewataka wananchi, watendaji pamoja na wabunge kuacha
kulalama kwa kutupa kila mzigo kwa serikali na kusema kuwa kila mtu kwa
nafasi yake anawajibu wa kuijenga Tanzania.
Kuhusu ubinafsishwaji, rais mstaafu Mkapa amesema hapakuwa na
tatizo katika zoezi hilo huku akikiri kuwa changamoto kubwa
iliyojitokeza ni ukosefu wa chombo cha kusimamia ubinafsishwaji huo,
ambapo pia amehoji licha ya serikali kufungua milango ya uwekezaji
lakini bado wafanyabiashara wa Tanzania wameshindwa kutumia fursa hiyo
na badala yake wameendelea kuwa walalamikaji.
Mwenyekiti wa kigoda cha Mwalimu Nyerere Prof Penina Mrama pamoja
na makamo mkuu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam Prof Rwekaza Mukandala,
wamesema kigoda cha Mwalimu Nyerere kimekuwa kikisaidia kuona namna
fikra pevu za mwalimu zinavyopaswa kuenziwa.
Katika siku ya kwanza ya kongamano la 8 la kigoda cha Mwalimu
Nyerere chenye kauli mbiu isemayo Mwalimu Nyerere na mtazamo wa
kimaendeleo uliojikita katika misingi ya watu, kilihudhuliwa na wasomi,
watu mashuhuri na wanadiplomasia, huku viongozi wa nchi za Afrika
wakitakiwa kuachana na tawala za kiimla na badala yake kujenga
utaratibu wa kuwasikiliza watawaliwa.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini