Wakizungumza na ITV baadhi ya wananchi wamesema uzimaji wa simu
feki hapa nchini wameupokea kwa mikono miwila ila walio wengi hawajui
nini maana ya simu feki huku wakiomba serikali kuwapatiwa elimu juu ya
bidhaa hiyo feki ambayo inatarajiwa kuzima siku ya juni 16 mwaka huu.
Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara wa simu mkoani hapa,
wamesema kuzima kwa simu feki ni jambo zuri lakini serikali inatakiwa
kudhibiti uingizaji wa bidhaa kwa sasa.
Naye mshauri wa masuala ya watumiaji, huduma na bidhaa za
mawasiliano kutoka TCRA, Isaac Mruma, amesema baada ya juni 17 mwaka huu
tume ya ushindani wa haki na polisi watapita kwenye maduka ya simu
kuangalia kama kuna wafanyabiashara ambao bado wanaendelea kuuza simu
feki na atakae kutwa sheria kali dhidi yake itachukuliwa.
Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA wanatarajia kuzima simu feki
ifikapo Juni 16 mwaka huu majira ya saa sita usiku, ambapo wananchi
wengi mkoani Lindi hawajui nini maana ya simu feki huku wakiomba
serikali kutoa elimu mikoani juu ya vifaa feki ambavyo vimekuwa
vikiingizwa nchini na wafanyabiashara mbalimbali.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini