Wananchi wakipatiwa maelezo juu
ya tofauti ya simu halisi (Original) na simu zisizo halisi (Fake),
kutoka kwa maafisa wa kampuni ya simu ya Vodacom wakati wa maonyesho ya
simu kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam, Juni 11,
2016.
Afisa
wa Vodacom huduma kwa wateja, Jesca Mnosi, akitoa maelezo ya simu
halisi na zisizo halisi kwa wananchi waliotembelea banda la Vodacom
kwenye maonyesho ya simu yaliyoanza jana Juni 11, 2016 kwenye viwa nja
vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Afisa wa Vodacom kitengo cha
huduma kwa wateja, Eunice Dominic, akimpatia maelezo mteja wa Vodacom
alipotembelea banda la kampuni hiyo ya simu kwenye maonyesho ya simu
orijino, Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam Juni 11, 2016.
Mtaalamu
wa simu wa Vodacom, Gabriel Mvamba, (kulia), akimpatia maelezo ya
kitaalamu ya kutofautisha simu halisi na simu isiyo halisi, mteja wa
kampuni hiyo alipotembelea banda la Vodacom kwenye maonyesho ya simu
orijino kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam, Juni
11, 2016.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini