Gareth Bale atamba kuibomoa Uingereza hii leo. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Thursday, June 16, 2016

Gareth Bale atamba kuibomoa Uingereza hii leo.


Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale amesema wanajua udhaifu wa Uingereza na watatumia mapungufu yao kuwafunga kwenye mchezo wa leo michuano ya Euro 2016 kwenye mji wa Lens.
Bale, aliyepiga mpira wa free-kick na kufunga bao katika mchezo wa kwanza wa kundi B na kushinda mabao 2-1 dhidi Slovakia, amesema hiyo ni mechi ya Derby na watajitoa kwa asilimia 100 kuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya Uingereza.
Nahodha wa Uingereza Wayne Rooey amesema hawachezi na Bale, bali wanacheza na Wales, hivyo watakuwa na umakini na wachezaji wote wa timu hiyo ili kushinda.
Wales haijaifunga Uingereza tangu mwaka 1984, lakini kwa sasa inajivunia kuwa inaweza kufanya maajabu hayo kwa nyota wao kama Gareth Bale (Real Madrid), Aaron Ramsey (Arsenal), Joe Allen (Liverpool) na Ashley Williams (Swansea City).
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin