Serikali
imewahakikishia Watanzania kuwa inaendelea kuweka utaratibu kuongeza
madawati na miundombinu ya vyumba vya madarasa nchini, kuhakikisha
wanafunzi wote wanaokaa chini na kurundikana madarasani, wanapata
madawati na vyumba vya kutosha.
Lakini,
imesema hawawazuii wadau mbalimbali ikiwamo watanzania, kuchangia
katika kuongeza miundombinu hiyo huku wabunge wakipongezwa kwa kuunga
mkono serikali kwa kuchangia madawati.
Waziri
Mkuu, Kassimu Majaliwa alisema hayo bungeni jana wakati akijibu maswali
ya papo na hapo na kueleza kuwa ni jukumu la serikali kumaliza
mirundikano hiyo na watafanyia kazi.
Waziri
Mkuu alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Mahawe
(CCM) aliyetaka kujua baadhi ya wananchi wanaodaiwa kulipa kodi mara
mbili na kutofaidika na sera ya elimu bure.
Akijibu swali hilo, Majaliwa alisema suala la elimu bure limekuwa likichanganywa na wakati mwingine kupotoshwa.
Alisema
elimu bure ni mkakati unaolenga katika elimu ya msingi na sekondari kwa
lengo la kuwapunguzia mzigo wazazi kwa kupunguza michango iliyokuwa
inawakwaza .
Alisema
wameanza na maeneo ambayo wameondoa ada kwa sekondari Sh 20,000 hadi
70,000, ulinzi, maji umeme na mitihani kwa kutenga fungu kuipa shule
kulipia ili wazazi wasipate mzigo wa michango na wanaendelea kuangalia
maeneo mengine wanayochangia ili kuwapunguzia mzigo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini