Wanaharakati na wanasiasa wanaobeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano, wametakiwa kuacha kuupotosha umma juu ya mafanikio yaliyofikiwa na Serikali hiyo chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Kauli
hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam leo na Afisa Habari wa CZI-
information And Media Consults Co. Ltd, Augustino Matefu wakati wa
mkutano na vyombo vya Habari uliolenga kueleza mafanikio ya Serikali ya
awamu ya tano.
Alisema
Serikali ya awamu ya tano imeonesha mafanikio makubwa katika sekta ya
ukusanyaji mapato, elimu, miundombinu, afya na kujenga uwajibikaji
miongoni mwa watumishi wa umma.
Hivyo
alitoa wito kwa Watanzania wote kuunga mkono juhudi za Serikali ya
awamu ya tano na kuwapuuza wanaharakati na wanasiasa hao wanaunga mkono
wale wasioitakia mema Tanzania na Serikali ya awamu ya tano kwa ujumla.
Alisema
katika sekta ya mapato, Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha
miezi saba iliyopita imefanikiwa kuongeza mapato kutoka shilingi bilioni
900 kwa mwezi kabla ya utawala wake hadi shilingi trilioni 1.5 kwa
sasa.
“Rais
wa awamu ya tano ameondoa michango yote ya shule za msingi na Sekondari
ambayo ilikuwa kero kwa wazazi na wananchi kwa ujumla” alisisitiza Matefu
Katika
mpango wa elimu bure Matefu alibainisha kuwa umesaidia kuongeza idadi
ya wanafunzi wanaoandikishwa kujiunga na elimu ya msingi na ile ya
Sekondari.
Aliongeza
kuwa Rais Magufuli amejenga Barabara ya Mwenge hadi Moroko kwa Fedha za
ndani hali inayoonyesha kuwa Serikali inayo dhamira ya dhati ya
kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Alisema
hata Hosipitali ya Taifa Muhimbili imepatiwa vitanda vya kutosha na
hivyo kuondoa tatizo la msongamano katika wodi ya wazazi na kwa sasa
wagonjwa wanalala kwenye vitanda.
“Mambo
mengine yaliyofanywa na Serikali katika kipindi hiki yanalenga kuinua
maisha ya wananchi wa chini ikiwemo kujenga mazingira mazuri
yatakayowezesha shughuli za uzalishaji kuongezeka ili kuinua hali ya
maisha ya wananchi” alisema Matefu.
Kujengwa
kwa utamaduni wa uwajibikaji miongoni mwa watumishi wa umma ni moja ya
mambo yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya tano ambapo sekta ya utumishi
wa umma imeonesha mabadiliko makubwa katika uwajibikaji.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini