Waziri
mkuu Kassim Majaliwa amesema kauli ya Rais John Pombe magufuli ya
kuzuia kuingizwa kwa sukari kiholela nchini ilikuwa ni katika kulinda
viwanda vya ndani.
Aidha
Majaliwa amesema kuingia kwa sukari Tani 70,000 toka nje ya nchi
hakutaathiri uzalishaji wa viwanda unaotarajiwa kuanza mapema mwezi
julai.
Akijibu
swali la kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni na mbunge wa jimbo la
Hai, Freeman Mbowe, Majaliwa amesema uhaba wa sukari ni tani 100,000 na
uwezo wa viwanda kuzalisha ni tani 320,000 huku mahitaji ya sukari kwa
mwaka mzima ni tani 420,000.
Amesema
katika kukabiliana na uhaba uliopo Serikali kupitia bodi ya sukari
imeagiza sukari nje ya nchi na tayari Serikali imeshaanza kupanga
mikakati ya kudumu ya kumaliza tatizo la sukari kwa miaka ijayo.
Akiuliza
swali la nyongeza Mbowe alimtaka waziri mkuu kuwahakikishia watanzania
kuhusu bei elekezi na kutaka kujua ni lini uraismu wa uanzishwaji wa
shamba/kiwanda eneo la bagamoyo utakavyo malizwa.
Akijibu
swali hilo Waziri Mkuu amesema swala la kuanzisha shamba katika eneo la
bagamoyo lina mchakato mrefu na halina urasimu wowote.
Amesema
shamba hilo limepakana na mbuga ya saadani na kwamba linategemea sana
maji ya mto Wami, lakini pia wanyama nao wanategemea maji ya mto huo.
Hivyo amesema serikali na wadau wanaendelea kuangalia suala hilo kwa umakini ili kutoa maamuzi yatakayo leta tija kwa taifa.
Kuhusu
bei elekezi ya sukari amesema tayari bodi ya sukari imeshaanza
kusimamiasuala hilo, ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua wale wote
watakaopandisha sukari kiholela
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini