Siku
chache baada mwananchi mmoja kuuawa kwa kupigwa risasi katika eneo la
Nyamongo wilayani Tarime, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mara
imetembelea eneo hilo na kutoa maagizo mazito kwa vyombo vya ulinzi na
usamlama wilayani humo kwa kutaka kukomeshwa mara moja mauaji hayo ya
Mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kudhibiti vitendo vya uvamizi wa mgodi
huo wa North Mara unamilikiwa na kampuni ya Acacia Gold Mine.
Akizungumza baada ya kujionea uharibifu mkubwa ambao umefanywa na
wananchi katika kituo cha afya cha Nyamongo wakati wa vurugu kati
ya polisi na wananchi muda mfupi baada mkazi mmoja wa kijiji cha Mrito
kuuawa kwa kupigwa risasi, mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama
mkoa wa mara Bw Magesa Mulongo, amesema haiwezekani wananchi kudai haki
kwa kuvunjwa kwa sheria.
Hata hivyo mwenyekiti huyo wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye
pia ni mkuu wa mkoa wa Mara, amemuagiza mkuu wa wilaya ya Tarime kuandaa
mafunzo maalum kwa vikundi vya ulinzi wa jadi maarufu kama Seiga kwa
kuzingatia sheria za nchi ili vitumike kwa shughuli za ulinzi katika
eneo hilo.
Awali viongozi na wananchi wa Nyamongo wamemuomba mkuu wa mkoa wa
Mara kukubali sasa kurejesha kwa ulinzi wa kutumia vikundi vya jadi
maarufu kama Seiga ambavyo wamesema vimekuwa na nafasi kubwa ya
kupambana na uhalifu katika eneo hilo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini