Rufani
ya aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’, Harry
Kitilya, Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa mwandamizi benki ya Stanibic
tawi la Tanzania ambaye pia ni mshindi wa taji la Miss Tanzania 1996,
Shose Sinare imesikilizwa leo Mahakama kuu.
Upande
wa utetezi umedai kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi
hiyo kwa kuwa mahakama ya hakimu mkazi kisutu haikumaliza kusikiliza
kesi hiyo lakini upande wa serikali umesema haki wanayo kwa sababu
shitaka la nane limeshamalizika.
Mahakama Kuu imeeleza kuwa kesho ndio itatoa uamuzi wa Rufani hiyo kama isikilizwe mahakamani hapo au la.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini