Mfanyabiashara Naila Aminel (24) amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya Sh milioni tano baada ya kukiri kutumia mtandao wa kompyuta kutuma ujumbe wa lugha ya matusi.
Aminel
ambaye ni mkazi wa Kariakoo, alihukumiwa kifungo hicho jana katika
Mahakama ya Wilaya ya Ilala, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi,
Said Mkasiwa.
Awali,
akisoma mashitaka, Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto alidai kuwa
mshitakiwa alitenda kosa hilo Februari 13 mwaka huu, maeneo ya katikati
ya jiji, wilayani Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam.
Mitanto
alidai kuwa mshitakiwa alitumia lugha ya matusi dhidi ya Martha Sebarua
kupitia mtandao wa kompyuta kinyume na kifungu namba 23 (1) na (3) cha
Sheria ya Makosa ya Mtandao namba 14 ya mwaka 2015.
Hata hivyo, Mitanto aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.
Mshitakiwa
huyo alidai hakumtukana mlalamikaji isipokuwa alifanya hivyo kwa kuwa
alimchukulia mume wake na walipiga picha za utupu na kumtumia kwenye
simu yake.
Aliiomba pia mahakama kumpunguzia adhabu kwa kuwa ana watoto wadogo ambao wanamtegemea.
Hakimu
Mkasiwa alisema kuwa mshitakiwa amekiri kutumia lugha ya matusi hafai
katika jamii na kwa sababu kosa lake ni la kwanza, atatakiwa kutumikia
kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya Sh milioni tano.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini