Shirikisho
la soka tanzania TFF limesimamisha mara moja mchakato wa uchaguzi wa
klabu ya Simba hadi hapo kamati ya utendaji ya Simba itakapo unda kamati
ya maadali.
Akizungumza na waandishi wa habari rais wa TFF
Jamal Malinzi amesema TFF imepokea malalamiko kadhaa juu ya ukiukwaji wa
maadili wa wagombea na wanachama kadhaa wa klabu ya Simba.
Malinzi amesema kwa mujibu wa katiba ya Simba ibara
ya 16 kifungu (e) na ibara ya 30 kifungu (h) kamati ya utendaji ya
Simba imeagiza iunde kamati ya maadili mara moja na kwamba kamati hiyo
ya maadili ikae mara tu baada ya kuundwa na kusikiliza mashauri yote ya
kimaadili ambayo kwa sasa yamewasilishwa TFF na walalamikaji kadhaa.
Aidha Malinzi amesema kwa mujibu wa kanuni za
uchaguzi za TFF ibara ya 2 kifunga cha (4) kamati ya utendaji ya Simba
itaendelea kuwa madarakani hadi hapo mchakato wa uchaguzi wa Simba.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini