16
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amewaambia watendaji na wadau wa mradi Mabasi
Yaendayo Haraka wa jijini Dar es Salaam (BRT) kuwa hawana muda wa kulala
kupumzika na akawataka wakamilishe haraka vipengele vichache
vilivyobakia ili mradi huo uweze kuanza kazi mapema iwezekanavyo.
Ametoa
agizo hilo juzi usiku (Ijumaa, Aprili 15, 2016) wakati akizungumza na
wakuu wa taaasisi, watendaji wakuu na wadau wa mradi huo kwenye kikao
alichokiitisha ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam.
“Watu
wa DART, UDA-RT hakuna muda wa kulala tena. Nanyi wa eGA, MAXCOM,
POLISI NA SUMATRA inabidi mfanye kazi kama timu moja na wenzenu ili
maeneo yaliyobakia yaweze kukamilika katika muda mfupi na kikubwa ni
kuhakikisha mnatoa elimu ya kutosha,” alisisitiza.
Akielezea
utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Bw. Ronald Rwakatare amesema miundombinu
ya mradi huo imekamilika na utoaji huduma unatarajiwa kuanza hivi
karibuni kwani hivi sasa wanamalizia ufungaji wa mfumo wa ukusanyaji
nauli na uendeshaji wa mabasi hayo.
Pia
aliwataka wananchi kutunza miundombinu ya mradi huo na kuwa makini na
matumizi ya barabara wakati mradi huo ukiwa kwenye majaribio na hatimaye
kuanza kazi rasmi.
Alisema
watakuwa na karakana itakayotumika kwa ajili ya hayo mabasi ambayo
itakuwepo eneo la Jangwani na kwamba ofisi za mradi pia zitakuwa eneo
hilo.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa UDA Rapid Transit (UDA-RT), Bw. Robert
Kisena amesema mpango wa kuanza kwa mradi huo umekamilika na tayari
mabasi yote yamelipiwa kodi pamoja na bima. UDA-RT ni kampuni ya
muunganiko wa UDA na wamiliki wa daladala ya kutoa huduma ya usafiri
katika miundombinu ya mabasi yaendayo haraka.
Bw.
Kisena amesema leo wataanza majaribio ya mradi huo kwa kutumia mabasi
10 na watakuwa wanaongeza mabasi 10 kila siku hadi yafikie 50 hivyo
amewataka wananchi kuondoa shaka juu ya mradi huo.
Naye,
Mkurugenzi Mkuu wa Maxcom Africa, Bw. Juma Rajab amesema mabasi hayo
yatakuwa yanatumia kadi za kielektroniki zitakazokuwa zinalipiwa kwa
kutumia mitandao mbalimbali ya simu za mkononi.
Bw.
Rajab amesema Tanzania inakuwa nchi ya kwanza kuanza kutumia mfumo huo
katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwamba fedha za mteja zitakuwa
salama na hata kama atakapopoteza kadi yake.
“Mtu
akinunua kadi yake anapaswa atunze namba ya usajili iliyoko kwenye kadi
hiyo kwani itatumika kurudishia fedha zake kupitia namba yake ya simu
ya mkononi,” alisema.
Amesema
Maxcom Africa ndio wakusanyaji wa nauli kwa kushirikiana na UDA-RT
ambapo watatumia mawakala wa MaxMalipo hivyo kila mwananchi atapata
fursa ya kununua kadi yake kwa urahisi.
Alisema
taarifa za kila mtumiaji zitaunganishwa na simu yake ya mkononi ambapo
mhusika ataweza kujua kwa urahisi salio la fedha lililomo kwenye kadi
yake.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini