Polisi watatu wa wilayani Urambo, Mkoa wa Tabora wamefikishwa mahakamani kwa mashitaka ya kuomba na kupokea rushwa.
Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Tabora, iliwafikisha
askari hao jana katika Mahakama ya Wilaya ya Urambo huku mwingine
akidaiwa kukimbia.
Askari hao waliofukuzwa kazi kabla ya kufikishwa mahakamani ni John Okinda, Kabila Pius na Patrick Robart.
Anayedaiwa kukimbia ni Elisha ambaye polisi inaendelea kumtafuta.
Mbele
ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Urambo, Hassan Momba,
Wakili wa Takukuru, Edsoni Mapalala alidai washitakiwa walitenda makosa
hayo Machi 7 mwaka huu.
Mapalala
alidai siku hiyo katika kijiji cha Mkirigi, Kata ya Ilege, Wilaya ya
Kaliua, washitakiwa hao wakiwa waajiriwa wa jeshi la polisi, waliomba
rushwa ya Sh milioni tatu kutoka kwa Dotto Gandulanye ili wasimchukulie
hatua za kisheria baada ya kumkuta akiwa na bangi.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini