Bosi wa zamani wa TRA na wenzake wawili waendelea kusota mahabusu. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Friday, April 8, 2016

Bosi wa zamani wa TRA na wenzake wawili waendelea kusota mahabusu.




Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es Salaam inatarajia kutoa maamuzi ya kupatiwa ama kunyimwa dhamana kwa watumiwa watatu akiwemo aliyekuwa kamishina mkuu wa TRA wanaokabiliwa na makosa manne likiwemo la utakatishaji wa fedha mapema April 22 mwaka huu.
Hati ya mashitaka inawataja watuhumiwa wote watatu kila mmoja akikabiliwa na mashitaka manne, huku mshitakiwa wa pili aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania mwaka 1996 akikabiliwa na mashitaka  mawili zaidi.
 
Wanasheria kutoka upande wa utetezi walikuwa na kazi moja ya kutumia vifungu vya sheria hasa sheria ya utakatishaji fedha, ili kuona namna wanavyoweza kuwanasua watuhumiwa hao kwa dhamana.
 
Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo Emilius Mchauru, jopo la utetezi kwa watuhumiwa hao likiongozwa Dkt Ringo Tenga, walipinga shitaka namba 8 la utakatishaji wa fedha amablo liliawsishwa na upande wa serikali kwa kutumia kifungu namba 12 A, na kuiomba mahakama kuruhusu kifungu hicho kusomwa kuanzia A hadi D, tofauti ilivyowasilishwa na mahakama.
 
Hata hivyo upande wa serikali kupitia kwa wakili wa mwanasheria mkuu wa seriakli Oswad, uliendelea kubaki na msimamo wake wa kusoma kifungu namba 12 A, pekee, jambo lililozua mvutano mkali wa kisheria, na hatimaye hakimu Mchauru akaiahirisha kesi hiyo hadi April 22 mwaka huu ili kutoa uamuzi kuhusu dhamana za watuhumiwa hao.
 
Katika shitaka la nane watuhumiwa hao wanakabiliwa na tuhuma za utakatishaji wa fedha kiasi cha Dola za Marekani 6 milioni, shitaka ambalo kisheria halina dhamana ambapo watuhumiwa wote wamerejeshwa lumande hadi april 22 mwaka huu.
 
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin