Mawasiliano ya Ifakara, Ulanga, Malinyi yakatika baada ya kuvunjika daraja la Mang'ula Morogoro. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Friday, April 8, 2016

Mawasiliano ya Ifakara, Ulanga, Malinyi yakatika baada ya kuvunjika daraja la Mang'ula Morogoro.



Wananchi wa wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi wameshindwa kuvuka upande mmoja kwenda mwingine baada ya kukatika kwa daraja linalounganisha barabara ya kutoka Morogoro kwenda maeneo hayo, katika eneo la Mang'ula A wilayani Kilombero, jambo lililosababisha adha kubwa kwa wasafiri wanaotumia barabara hiyo.
Hali hiyo imejitokeza baada ya kunyesha kwa mvua kubwa hali iliyosababisha wasafiri na watumiaji wengine wa barabara hiyo kushindwa kuvuka upande mmoja kwenda mwingine ambapo baadhi ya wananchi wamesema daraja hilo limekatika kutokana na uchakavu kutokana na kujengwa kwa muda mrefu, na limekuwa likipitidha mizigo yenye uzito mkubwa na kwamba mara kwa mara maeneo hayo yamekuwa na kero sugu ya kukatika kwa mawasiliano kutokana na uharibifu wa miundombinu ya barabara bila kupatikana suluhisho la kudumu.
 
Wasafiri walio kwama katika eneo hilo wameeleza kusikitishwa na hali hiyo kwani wamekwisha toa taarifa mapema kwani walitoa taarifa kwa mamlaka mbalimbali bila mafanikio na kwamba madhumuni yao ya kibiashara na shughuli binafsi yamejikuta yĆ kikwama na kutumia fedha za matumizi mengine kujikimu na kusababisha hasara.
 
Msemo wa kufa  kufaana ulidhiirika pale ambapo wafanyabiashara za vyakula na wasafirishaji wa abiria kwa kutumia pikipiki maarufu kama bodaboda waliipoonekana kufurahia hali hiyo kwa madai imewawezesha kujipatia kipato kibwa hivyo kuomba hali hilo kuendelea ili kupata fedha.
 
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin