Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga ukikamilika utaliingizia Taifa Sh4.8 bilioni kila siku.
Amesema
fedha hizo zitatokana na usafirishaji wa mapipa 200,000 kila siku
yatakayotozwa dola 12.2 (zaidi ya Sh24,000) kila moja.
Profesa
Muhongo alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari mara
baada ya kuwasili nchini akitokea Kampala ambako Rais wa Uganda, Yoweri
Museveni juzi alitangaza kuwa bomba hilo la mafuta ghafi kutoka Hoima,
Ziwa Albert litapita katika ardhi ya Tanzania kwenda Bandari ya Tanga.
Alisema
katika kujipanga kwa ajili ya mradi huo, tayari Serikali imetoa kibali
kwa wanafunzi 22 ambao wamepelekwa nje ya nchi kusomea masuala ya mafuta
na gesi katika ngazi ya Shahada ya Uzamili na Uzamivu.
“Bomba
litakamilika Juni 2020 na itakuwa ni zawadi kwa Rais John Magufuli
kabla hajarudisha fomu ya kuomba tena kugombea awamu ya pili ya urais.Lakini tutajitahidi likamilike kabla ya muda huo,” alisema Profesa Muhongo.
Alisema utakapokamilika, yatahitajika magari 100,000 ya kutolea mizigo katika Bandari ya Tanga.
Juzi,
taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Kikanda na Kimataifa ilieleza kuwa Serikali ya Uganda
imetangaza rasmi uamuzi wa kutumia Bandari ya Tanga.
Rais
Museveni alitangaza uamuzi huo wakati wa mkutano wa 13 wa Ushoroba wa
Kaskazini uliomalizika jijini Kampala juzi na kuhudhuriwa na Waziri wa
Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk
Augustine Mahiga na Profesa Muhongo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini