Mgogoro wa wananchi na mwekezaji Serikali yaombwa kuingilia kati Kilombero. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Tuesday, March 1, 2016

Mgogoro wa wananchi na mwekezaji Serikali yaombwa kuingilia kati Kilombero.

Wananchi wa kijiji cha Katulukila kata ya mkula wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro wameiomba serikali kuingilia kati mgogoro uliopo baina yao na mwekezaji aliyevamia hekari zaidi ya 500 za msitu wa hifadhi ya Magombera unaomilikiwa na kjiji hicho chini ya mamlaka ya uhifadhi wanyamapori ya Selou.
ITV imefika katika kijiji cha katulukila na kushuhudia uharibifu uliofanywa na mwekezaji huyo ambaye amekuwa akifanya shughuli za kilimo cha mpunga,upasuaji wa mbao pamoja na uchomaji wa mkaa ambapo wananchi wamelalamikia serikali kushindwa kuonesha jitihada za kunusuru hifadhi hiyo.
 
Naye mhifadhi  mkuu wa kanda ya Msolwa Agustino Ngamilanga amesema mamlaka haitavumilia kuendelea kufanyika uharibifu wa hifadhi hiyo kwani inahifadhi viumbe adimu ambavyo havipatikani mahali pengine duniani.
 
Akijibu malalamiko ya wananchi hao mwekezaji wa shamba hilo amesema anamiliki kihalali shamba hilo na kwamba wakati anaendelea na uzalishaji katika eneo hilo kesi ya msingi inayohusu mgogoro wa shamba hilo inaendelea katika baraza la ardhi la wilaya ya Kilombero.
 
 
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin