ITV imeshuhudia mbao hizo zikiwa tayari zimefikishwa katika makao
makuu ya polisi kikosi cha wana maji huku vijana waliokuwa wakisafirisha
mbao hizo kutokea Rufiji kuelekea visiwani Zanzibar nao wakiwa
wameshikiliwa na jeshi hilo ambapo kamanda wa kikosi cha wana maji
nchini kamishna msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi Mboje John Kanga
ameeleza walivyofanikiwa kukamata mbao hizo.
Aidha kamanda kanga, amewataka wenye tabia ya kusafirisha mizigo ya
aina yeyote kwa kutumia njia ya bahari au ziwa kinyemela ili kukwepa
kodi kuacha mara moja kwani hata majira ya usiku jeshi hilo ufanya kazi
zake baharini na kwenye ziwa.
Meneja misitu kutoka wakala wa misitu wilaya ya Ilala Bwana Doto
Ndubikwa amesema iwapo mwenye mali hiyo hatajitokeza kwa kipindi
kilichowekwa basi mali hiyo itataifishwa kwa maslahi ya umma huku vijana
hao walioshikiliwa wakieleza walivyokuwa wakisafirisha mbao hizo na
kwamba mwenye mali anaitwa Temri huku wakieleza malipo waliyoahidiwa.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini