Wenye vyomba vya moto watakiwa kuepuka stika feki za bima mkoani Iringa. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Sunday, January 31, 2016

Wenye vyomba vya moto watakiwa kuepuka stika feki za bima mkoani Iringa.

Mamlaka ya usimamizi wa shughuli za bima (TIRA)kanda ya nyanda za juu kusini imewataka madereva na wamiliki wa vyombo vya moto kuacha mtindo wa kununua na kubandika stika bandia za bima kwenye vyombo vyao kwani utaratibu huo hauwasaidii kutimiza malengo ya kuwekwa kwa sheria ya fidia kwa vyombo hivyo na wateja wao mara wanapopata majanga ya ajali.
Rai hiyo imetolewa na meneja wa mamlaka hiyo kanda za nyanda za juu kusini Bwana Hilard Maskini wakati akizungumza na waendesha bodaboda mjini Iringa ambapo amesema lengo la kutungwa kwa sheria hiyo ni kuhakikisha hasara yoyote inayoweza kutokea ama kusababishwa na chombo cha moto inafidiwa kwa mujibu wa bima iliyokatwa na mmiliki wa chombo husika ikiwa ni pamoja na kufidia chombo chenyewe inapobidi. 
 
Baadhi ya madereva wa bodaboda wameitaka mamlaka hiyo kuweka kipengere cha sheria kinachowalazimisha wenye makampuni ya bima nchini kutoa elimu kwa wateja wao badala ya kuwauzia huduma hiyo bila kutoa elimu yoyote jambo ambalo wamedai siyo msaada kwao. 
 
Kwa upande wake mmoja wa wakaguzi wa vyombo vya moto kutoka jeshi la polisi mkoani Iringa Inspecta Ramadhani Mgeni amewataka madereva wa vyaombo vya moto kuhoji mambo mbalimbali wanapokata bima na pia kujitokeza kwenye mikutano mbalimbali ya utoaji elimu ili waweze kupata elimu zaidi.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin